0
KWANINI MTU AKICHAGULIWA KUWA PAPA HUWA ANABADILISHA JINA?
KWANINI MNAMWITA PAPA "BABA MTAKATIFU",JE NI KWELI YEYE NI MTAKATIFU?

Pengine wakati fulani umeulizwa maswali hayo.Na majibu yake ni kama ifuatavyo:
1.MAMLAKA YA PAPA INAPATIKANA WAPI KATIKA BIBLIA?
-Inapatikana katika Mathayo 16:18-19,Luka 22:31-32,Yohane 21:15-17 nk.
Mathayo 16:18-29
"Nami nakuambia,Wewe ni Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu,wala milango ya kuzimu haitalishinda.Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni na lolote utakalofunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni,na lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni"
Luka 22:31-32
"Akasema,Simoni,Simoni,tazama shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;lakini mimi nimekuombea wewe ili imani yako isipungue,nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako"
Yohane 21:15-17
"Basi walipokwisha kula,Yesu akamwambia Simoni Petro 'Simoni Mwana wa Yohana,je wanipenda kuliko hawa?,Akamwambia Naam Bwana nakupenda;akamwambia lisha kondoo wangu.Akamwambia tena mara ya pili,Simoni Mwana wa Yohana,wanipend
a?Akamwambia ndiyo Bwana,wewe wajua kuwa nakupenda.Akamw
ambia,Chunga kondoo zangu.Akamwambia tena mara ya tatu,Simoni mwana wa Yohana,wanipend
a?Petro akahuzunika kwavile alivyomwambia mara ya tatu 'wanipenda'.....akamwambia lisha kondoo wangu"
Yesu alimchagua Simoni Petro kuwa kiongozi mkuu na wa kwanza wa kanisa lake.Tangu hapo utumishi huo(kiti hicho)umekuwa ukirithiwa bila kukatisha mpaka leo hii ambapo tunaye Papa Francis ambaye ni papa wa 266 tangu Petro.
Tukisema kwamba kauli ya Yesu ilimlenga Petro pekee basi ingembido huyo Petro asife kabisa bali aishi milele maana angekufa basi na kanisa nalo lingekufa kwani halina mchungaji.
Lengo la Yesu lilikuwa ni kutunza umoja wa kanisa lake,hivyo Petro,yaani Papa ni ishara ya umoja huo.
2.KWANINI MTU AKICHAGULIWA KUWA PAPA HUBADILISHA JINA?
~Ni kwasababu ya ukuu wa utume anaouchukua.Ni ili awe mtu mpya na aweze kutekeleza kazi hiyo kama somo wake.
Lakini Pia ni kwasababu Yesu mwenyewe alipompa Simoni utume huo,alimpa jina jipya(Marko3:16,Mathayo 16:18)na hivyo kanisa Katoliki(kwasababu asili yake ni mitume)hubadili jina wakati mtu anapokuwa Papa na hivyo huwa na jina jipya kabisa.
Marko 3:16
"Akawaweka wale Thenashara na Simoni akampa jina la "PETRO"
Ikumbukwe kuwa,Petro mwanzoni aliitwa SIMONI na jina PETRO alipewa na Yesu mwenyewe ambalo lilitokana na neno "PETRA" Likiwa na maana ya "Mwamba"
Mathayo 16:18
"Nami nakuambia,wewe ni PETRO na ju ya MWAMBA huu nitalijenga kanisa langu"
3.KWANINI MNAMWITA PAPA "BABA MTAKATIFU",YEYE NI MTAKATIFU?
~Jina hilo linadokeza yale mambo makuu anayoyasimamia,Papa anasimamia "MAMBO MATAKATIFU".
anaweza kuwa Mtakatifu au asiwe mtakatifu,hiynategemea na bidii yake mwenyewe(1Wakorintho 9:16-27)
1Wakorintho 9:26-27
"Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo,si kama asitaye,napigana vivyo hivyo si kama apigaye hewa bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha,isiwe nikiisha kuwahubiria wengine,mimi mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa"
Lakini vilevile anayo nafasi nzuri zaidi ya kuwa Mtakatifu kwa ule ukaribu alionao na Mungu katika utume wake huo Mtakatifu.
Nimeipenda, nikapenda na wewe uipate!
TUMSIFU YESU KRISTO!




By Fr.Andrew Lupondya

Chapisha Maoni

 
Top