Papa alinukuu
kama ilivyoandikwa katika Injili ya Matayo , Maskini Lazaro daima
alipenda kulala mbele ya lango kuu la nyumba ya tajiri, akitamani
hata kula makombo ya chakula yaliyokuwa ya kidondoka kutoka meza ya
tajiri . Tajiri alivaa nguo anasa, wakati Lazaro alijifunika mwili wake
uliokuwa umejaa vidonda kwa matambara yaliyochokaa. Tajiri kila siku alikula na
kusaza wakati lazaro akifa kwa njaa , wala hakuwa na mtu wa kuhudumia
madonda yake badala yake mbwa walikuja kulamba madonda yake .
Baba Mtakaifu amesema,
mfano huu wa Lazaro na tajiri , unatukumbusha maneno makali ya ujio
wa pili wa Yesu , ambamo alisema siku ya mwisho wa hukumu , Mwana
wa Mtu atakapokuja tena kuwachukua walio wake na wasio wake atawaambia
”Mimi nilikuwa na njaa hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu nanyi hamkunipa maji,
nilikuwa [...] uchi hamkunivika " ( mt 25.42-43)”.
Papa anasema mfano wa
maisha ya watu hawa wawili unatonyesha kwamba , Lazaro anawakilisha
vizuri kilio cha kimya kimya cha baadhi ya maskini wa wakati wote
na hali tata za ulimwengu ambamo utajiri mkubwa wa rasilimali
za dunia umeshikwa na mikono ya wachache.
Papa ameendelea kueleza
ilivyokuwa kwa watu hawa wawili Lazaro na Tajiri walipokufa . Tunasoma
kwamba kukawa na mageuzi makubwa , aliyekuwa maskini anakuwa tajiri na
tajiri anakuwa maskini. Lazaro anapa kutuzwa mbele ya uso wa Mungu na kuchuliwa
na malaika na kulazwa katika kifua cha baba wa Imani Abraham .
Wakati mtu tajiri,
alyeijiona amejitosheleza mwenyewe hapa duniani na kudharau ya Mungu ,
sasa anatupwa jehanamu katika mateso makali ya njaa akitamani hata
tone la maji lidondoke ulimini mwake, kutuliza kiu yake .
Lakini Abraham anamweleza kwa jinsi gani , utendaji wa haki
na huruma inavyokuwa kutimiza fumbo Takatifu la Mungu
linavyohusiana na husiana na matendo ya huruma na kwa wengine .
Papa aliendelea kuonya
kwamba, kama ilivyokuwa kwa mtu huyo tajiri, milango ya mbingu imefungwa
kwa wale ambao mioyo yao haiguswi na mahitaji ya watu maskini.
Baada kifo na kutupwa jehananu mtu huyu tajiri ndipo anayafungua macho
yake na kumwona Lazaro uwinginimikononi mwa Abrahamu. Tajiri huyo
anajaribu kuomba msaada lakini anaambiwa amachelewa . Hivyo kumbe Papa anasema
wakati ni huu wa wa wogofu , wakati wa kufungua mioyo na kuuona ukweli wa neno
la Mungu na ujumbe wake wa kuokoa , kama alivyoimba Mama Yetu Bikira
Maria katika wimbo wake mkuu . Ni kufanya mabadiliko katika maisha ya
dunia hii kwa ushindi wa haki na huruma ya Mungu. Na wogofu
wetu tusiuegemeze katiak miujiza , bali tufungue mioyo yetu wai kwa neno la
Mungu anayetutaka tumpende yeye na jirani zetu.
BabaMtaktifu alikamilisha
Katekesi yake kwa maneno kwamba, Neno la Mungu lina nguvu ya kuuinua moyo
uliopondeka na kuuponya upofu wake . Na kwamba Ujumbe wa Mungu wa una uwezo wa
kuibadilisha sura ya dunia hii kwa ushindi wake wa haki na huruma.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni