0
MASOMO YA MISA, MEI 30, 2016
JUMATATU YA 9 YA MWAKA SOMO 1 2Pet. 1:2-7 Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu. Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika sabauri yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na ktika upendano wa ndugu, upendo. Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu. WIMBO WA KATIKATI Zab. 91:1-2, 14-16, (K) 2 (K) Mungu wangu ninakutumaini. Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. (K) (K) Mungu wangu ninakutumaini. Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu. Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, kw akuwa amenijua jina langu. Ataniita nami nitamwitikia. (K) Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu. (K) SHANGILIO Zab. 130:5 Aleluya, aleluya. Roho yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelitumainia. Aleluya. INJILI Mk. 12:1-12 Yesu alisema na Mafarisayo kwa mifano; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akazungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Hata kwa wakati wake akatuma, mtumwa kwa wale wakulima, ili apokee kwa wakulima katika matunda ya mizabibu. Wakamtwaa, wakampiga, wakamtoa nje, hana kitu. Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, na huyo wakamtia jeraha -za kichwa, wakamfanyia jeuri. Akamtuma mwingine, huyo wakamwua; na wengine wengi, hawa wakiwapiga na hawa wakiwaua. Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu. Wakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu. basi atafanyaje yule bwana wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine. Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni. Neno hili limetoka kwa Bwana, nalo ni ajabu machoni petu? Nao wakatafuta kumkamata, wakaogopa mkutano; maana walitambua ya kwamba ule mfano amewanenea wao. Wakamwacha wakaenda zao. Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo. [5/29, 22:02] Nyambane Maurice: “ASALI ITOKAYO MWAMBANI” Jumatatu, Mei, 30, 2016, Juma la 9 la Mwaka wa Kanisa 2 Pet 1: 2-7; Zab 90: 1-2, 14-16; Mk 12: 1-12 MUNGU ANAYETUJALI (MWEMA)! Fumbo tulilo nalo leo kwa tafakari yetu ni kuhusu muonekano wa uzuri na wema wa Mungu. Jinsi Mungu anavyotenda na jinsi mwanadamu anavyofikiri ni vitu viwili tofauti kabisa kiasi ambacho mwanadamu anajiandaa akidhani atashambuliwa. Wema haujajikita katika kutoa mengi tu, bali kutoa hata kidogo kwa wakati. Mungu alimtoa mwanaye kwawakati kwaajili yetu. Alitupa yote kwa wakati. Yesu aliongea na kutenda katika hali ambayo watu kwakuona anayosema nakutenda, wakatambua Mungu ni wa namna ghani. Kwa maneno mwengine, Yesu hakuongea tuu kuhusu Mungu na kuonyesha muelekeo wa kwenda kwake, bali alionesha uwepo wa Mungu na Mungu akaonekana akiwa kati ya watu wake. Kama sio yeye, Mungu kwetu angekuwa ni kama kitu tuu cha kutumaini nakutafuta. Lakini kwa njia yake Mungu yupo kati yetu (Ekaristi Takatifu). Kabla ya Yesu, hakuna aliyejua sifa za Ufalme wa Mungu ulivyo, yeye ndiye aliyetupa mifano akielezea jinsi Ufalme wa Mungu ulivyo, na akatuambia yeye amekuja kuutangaza, upo kati yetu, nabado utatimilizwa katika maisha ya umilele. Kwahiyo tukiishi vizuri na wengine tunaishi Ufalme wake tukiwa hapa duniani. Yesu, hakutaka chochote kwaajili yake binafsi, bali kila kitu alichokuwa nacho na kutenda, alifanya kwaajili yawengine. Kila mmoja wetu ni wa Yesu, chombo cha upendo wa Mungu, na chombo chakupokea wema wa Mungu. Leo tujiulize kama tumekuwa wazi kwa wema na upendo huu wa Mungu. Sala: Nisaidie Bwana, niweze kuutambua wema wako ili niweze kuwa mwema. Amina.

Chapisha Maoni

 
Top