0
Baada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kunaswa na kamera akiidunisha Nigeria kuwa mafisadi wakuu kote duniani BBC imeamua kuangazia kwa umakini ikiwa matamshi hayo ni ya kweli.

Je Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ipi katika orodha ya mataifa fisadi kwa mujibu wa shirikisho la kupambana dhidi ya ufisadi duniani Transparency International ?

Ni vigumu kuelezea kwa kina ama hata kupiga msasa ufisadi katika mataifa kwani kila mwanauchumi anaelezea ufisadi akitumia mizani tofauti na mwenziye.
Kwa sababu hiyo tutatumia orodha ya mwaka wa 2015 ya shirikisho la kupambana dhidi ya ufisadi, Transparency International, ili kukupa taswira ya mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na jinsi yanavyolinganishwa na mataifa mengine duniani katika mizani ya ubadhirifu na wizi wa mali ya uma.
Cha mno hata hivyo sharti tuweke bayana kuwa Nigeria sio taifa fisadi zaidi duniani.

Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ya 136 Nigeria kati ya mataifa 167.
Kenya kwa mfano inasemekana kuwa na ufisadi mkubwa hata kuishinda Nigeria.
Image copyrightAPImage captionZimbabwe wanaorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani kwa ufisadi.
Katika kanda ya Afrika Mashariki , mali ya umma inafujwa sana na viongozi wa serikali hali ambayo inaiweka mataifa ya kanda katika nafasi za mwisho mwisho kuashiria viwango vya juu vya ufisadi.
Kati ya mataifa kumi Fisadi zaidi duniani Somalia inaongoza ikifwatwa na Sudan ,Sudan Kusini, Eritrea, Burundi, DRC, Uganda, Kenya Tanzania Ethiopia na kisha Rwanda katika usanjari huo.
Somalia inaongoza kwa Ufisadi duniani katika nafasi ya 167.
Viwango vya ufisadi vinanasibishwa na Korea Kaskazini.
Nchi iliyojitenga kabisa na ufisadi kanda ya Afrika Mashariki na kati ni Rwanda.
.
Taifa hilo linaloongozwa na rais Paul Kagame linaorodheshwa katika nafasi ya 44 duniani.
Je unakumbuka rais Robert Mugabe aliyewadunisha wakenya kwa kuwa wezi ?
Kulingana na orodha hii iliyotayarishwa na shirika la TI Zimbabwe wanaorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani kwa ufisadi.
Wanagawana nafasi hiyo na Burundi.
Orodha ya mataifa 10 fisadi zaidi kanda ya Afrika Mashariki na Duniani.
1. 167 Somalia / Korea Kaskazini
2. 165 Sudan
3. 163 South Sudan/ Angola
4. 154 Eritrea/Yemen / Turkmenistan / Syria
5. 150 Burundi / Zimbabwe
6. 147 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo / Chad / Myanmar /
7. 139 Kenya / Uganda
8. 117 Tanzania
9. 103 Ethiopia
10. 44 Rwanda


Chapisha Maoni

 
Top