Papa
Francis ameongoza majadiliano ya kina hapo jana juu ya jukumu la wanawake
kanisani akisema
anaangalia
uwezekano wa kuanzisha tume ya kuchunguza uwezekano wa kurejesha
mashemasi
wa kike.Mazungumzo yake ilikuwa ni sehemu ya swali katika kikao cha
pamoja
na baadhi ya viongozi 900 wa umoja wa wanawake wa kanisa ambao ni sehemu
ya
Umoja wa Kimataifa uitwao UISG.Hata hivyo jambo hilo la kihistoria
haliwaruhusu
wanawake kuongoza misa bali watasimamia ubatizo,sala na mambo
mengine.Haya
yatakuwa mageuzi makubwa katika KARNE nyingi zilizopita huku
katika
karne ya 1 wanawake waliwahi kupewa nafasi hizo ila wakaacha.
Papa aruhusu mjadala wa wanawake mashemasi
Papa aliahidi kubuni tume kutafiti na kujadili uwezekano huo wa
kuwezesha wanawake kuhudumu katika ngazi hiyo ambayo ni daraja moja tu chini ya
makasisi. Wanahistoria wanasema zamani wanawake walihudumu kama mashemasi.
Papa
Francis akiwa Vatican.
Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amesema ataunda
tume itakayochunguza na kujadili uwezekano wa wanawake kuteuliwa kuwa mashemasi
katika Kanisa hilo katika pendekezo linaloashiria uwazi wa kuruhusu wanawake
kuteuliwa kuhudumu katika nafasi ambazo zimekuwa za wanaume pekee. Wazo hilo
tayari limeanza kuibua hisia mbalimbali.
Ni katika mkutano wake maalum na waumini wanawake 900
waliojumuika Vatican ambapo katika awamu ya maswali, suala hilo likaibuka. Papa
aliulizwa ikiwa atakuwa radhi kuruhusu utafiti kufanywa kuhusu uwezekano wa
wanawake kuwa mashemasi, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za sheria za kanisa
hilo. Papa aliahidi kubuni tume kutafiti na kujadili uwezekano huo wa kuwezesha
wanawake kuhudumu katika ngazi hiyo ambayo ni daraja moja tu chini ya makasisi.
Wanahistoria wanasema zamani wanawake walihudumu kama mashemasi.
Robert Gahl ambaye pia ni kasisi na pia profesa wa maadili
katika chuo kikuu cha kikatoliki Pontifical University of the Holy Cross
anasema "Kile ambacho Papa anatafakari ni uchunguzi wa kihistoria kuhusu
majukumu ambayo mashemasi wanawake walikuwa wakifanya, na kufikiria
kuyazingatia ili kuwezesha wanawake katika njia moja ya ushemasi. Hata hivyo
tutarajie kuwa papa hatahimiza kitu kama hicho kwa sababu tayari ameshasema hataki
wanawake kuwa makasisi. Analotaka ni kuwezesha wanawake katika jamii".
Wanawake waunga mkono
Wanawake kanisani maarufu Sisters.
Kauli ya Papa ilipokelewa vema na baraza la kutawaza wanawake
WOC, shirika la Marekani linalohimiza kanisa katoliki kuanza kutea na kutawaza
wanawake katika ngazi zote za huduma kanisani ikiwemo ukasisi. Papa Francis
ameonekana mara kwa mara akihimiza usawa wa kijinsia. Kate Mc Elwee ambaye ni
mkurugenzi wa baraza la uteuzi wa wanawake, ni kati ya wale ambao wamesifia
kauli ya Papa kwa kukubali mjadala huo ufanywe. Amesema "Ninafikiria kuwa
Papa kweli anataka swali hilo lijadiliwe. Maandiko yetu wenyewe na wahubiri
wametuambia kuwa wanawake sawa na wanaume wamekuwa mashemasi tangu zamani, kwa
hivyo ninafikiria tume itaunga mkono historian a itakuwa bora ikiwa Vatican
itakubaliana na hilo"
Mashemasi hutawazwa kuwa wahudumu tu wa kanisa lakini si
makasisi. Japo wanaweza kutekeleza majukumu mengineyo yanayofanywa na makasisi,
kama vile kuongoza sherehe za harusi, ubatizo na hata kuhubiri, hawawezi
kuongoza misa ya Pasaka.
Kadhalika amerudia mara kwa mara kuwa hataki kuwakilisha mafunzo
yote ya kanisa kana kwamba yameandikwa kwenye jiwe. Amejaribu kufanya kanisa
kuwa na uelawa na kutofanya maamuzi dhidi ya waliotalikiana, wanaowekeana
kimada na waumini ambao ni wapenzi wa jinsia moja
Mwandishi: John Juma/RTRE/AFPE
Mhariri:
Mohammed Khelef
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni