Alizaliwa Mwazye (mkoa
wa Rukwa) tarehe 5 Agosti 1944.Baada ya masomo ya ngazi. Kisha
kufundisha somo hilo kwa muda mfupi kwenye seminari kuu ya Kipalapala (mkoa
wa Tabora), alichaguliwa kuwa gombera wa seminari kuu ya Segerea hadi
mwaka 1983.
mbalimbali, alipewa upadrisho mwak 1971 na askofu Charles
Msakila wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga, akasoma teolojia ya maadili huko Roma, Italia,
akijitwalia digrii ya udaktari mwaka 1977
Aliteuliwa askofu wa Nachingwea tarehe 11
Novemba 1983, akapewa daraja
takatifu hiyo na Papa Yohane Paulo II tarehe 6 Januari 1984.
Tarehe 17 Oktoba 1986 alihamishiwa jimbo jipya
la Tunduru-Masasi.
Tarehe 22 Januari 1990 alifanywa askofu
mwandamizi wa Dar-es-Salaam na mwaka 1992, kardinali Laurean
Rugambwa alipojiuzulu, akawa askofu mkuu.
Aliteuliwa na Yohane Paulo II kuwa
kardinali tarehe 21 Februari 1998, akikabidhiwa parokia ya Nostra
Signora de La Salette mjini Roma.
Pamoja na majukumu mbalimbali
katika idara za Papa, tangu mwaka 2007 hadi 2013 alikuwa
mwenyekiti wa Umoja wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Afrika na
Madagaska.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni