Papa alieleza kwa kutazama kwa kina maneno ya Yesu kwa wanafunzi wake , wale ambao Yesu aliwaita na kuwataka wamfuate , na kushikamana nae kama jamii moja na kama familia moja, na wote walioalikwa harusini. Papa ametoa ufafanuzi juu ya tukio hili la Arusi ya Kana ambako Yesu alianza huduma yake ya hadharani, akisema, katika harusi ya Kana, inamwonyesha Yesu mwenyewe kuwa ni bwana harusi kwa watu wa Mungu, kuwa ndiye Yeye aliyetangazwa na manabii, napia inaonyesha uhusiano kina unaotuunganisha nae, ambalo ni agano jipya la upendo.
Papa aliendelea kueleza juu ya msingi wa imani yetu, akiswema ni tendo la huruma inayoonyeshwa na Yesu. Na hivyo maisha ya Kikristo, yanakuwa ni jibu lenye kuonyesha upendo huu,kama ilivyo historia ya watu wawili waliopendana. Katika upendo huo, Mungu na mwanadamu wanakutana, na kufurahi kwa upendo, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Wimbo ulio bora. Papa anasema upendo ni msingi na mengine yote ni matokeo ya upendo huo. Kanisa ni familia ya Yesu ambamo ndani mwake hutoka upendo wake;na ni upendo huo ambao Kanisa linaendelea kuutoa kwa kila mtu.
Papa alieleza na kurejea pia maneno ya Mama Maria akimwambia Yesu “Hawana divai", akitazama kwa jinsi kinywaji kilivyokuwa na umuhimu wake katika karamu yoyote ile. Alitaja umuhimu wa Maji katika maisha, na pia kwa jinsi mvinyo huonyesha furaha na kufana kwa sikukuu. Na kwamba, kugeuza maji yawe mvinyo katika maana ya kiluturujia hutumika kama msamiati wa kutakaswa kwa Wayahudi. Yesu anafanya ishara hii kwa uwazi katika maana ya kukamilisha sheria ya Musa katika injili ya furaha, kama Mwinjilisti Yohana alivyoandika: “Sheria ilitolewa kwa njia ya Musa, lakini neema na ukweli vimekuja kupitia kwa Yesu Kristo”.
Aidha Papa alirejea maneno ya Maria kwa Watumishi“fanyeni Lolote atakalowaambieni"akisema maana yake, kumtumikia Bwana ni kusilikiza na kutenda kwa agizo la neno lake. Fanyeni kama atavyowaambia, unakuwa ni mpango wa maisha kwa ajili ya utumishi wa kanisa.
Papa alikamilisha na wito akisema kuwa ndivyo wote tumeitwa katika kufanya upya upendo wetu kwa Bwana, kuchoka mvinyo mpya kutoka kwake , ambayo ni maisha mapya kutoka katika madonda yake ya kukomboa. Muujiza huu wa Kana , unatoa mwalko kwetu wote kama familia ya Bwana , ambalo ni kanisa lake kuwa katibu naye katika imani na hivyo kushirikishana furaha za agano jipya la milele.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni