Jumatano hii majira ya saa nane za Italia, Baba Mtakatifu alielekea Krakow Poland tokea uwanja wa ndege wa Fiumicino Italia , kwa ndege ya Altalia AZ/A321,safari ya saa mbili hewani akipita katika anga za Italia, Croazia, Slovenia, Austria , Slovakia na hatimaye kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Yohane Paulo II wa Balice umbali wa kilomita 11 kutoka Mji wa Krakow. Hii ni ziara ya Kitume ya Kimataifa ya 15 tangu awe Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ulimwengu.Katika kila taifa alimopita alitoa salaam zake matashi mema kwa wakuu wa Nchi na wanachi kwa ujumla. Kwa Rais wa Italia Mheshimiwa Mattarella Sergio, aliaga akisema , ninakwenda Poland nikiwa nimehamasika na kukutana na vijana kutoka pande mbalimbali za dunia, kwa ajili ya tukio la Siku ya Vijana ya Dunia, Mkutano muhimu unaofanyika chini ya Ishara ya imani na Udugu. Kwa moyo wa upendo na udugu nakusalimu wewe na raia wote wa Italia, nikiwaaombea wote amani na ustawi, nami nawaomba msisahau kuongozana nami kwa njia ya maombi. Na ndivyo ilivyokuwa kwa kila anga la Nchi alimopita alipeleka salaam zake za matashi mema na kuomba wamsindikize kwa na sala na maombi.
Mara baada ya kutua katika uwanja huo, alipokewa kwa heshima ya gwaride la wanajeshi, na kupokewa toka ndani ya ndege na mwakilishi wake nchini Poland , Askofu Mkuu Celestino Migliore, Askofu wa jina wa Canosa , na pia mkuu wa Portokali wa Poland, na Rais wa Jamhuri ya Poland Andrezej Duda pamoja na Kardinali Stanslaw Dziwisz, Askofu Mkuu wa Krakow na watoto wawili kama ishara ya upendo, pamoja na viongozi wengine wa kiserikali na kikanisa.
Jumanne majira ya saa moja za jioni , kama ilivyo desturi yake kabla ya kufunga safari ndefu ya kitume ya nchi za nje, Baba Mtakatifu Francisko, alikwenda katika Kanisa Kuu la Maria Mkuu , kutolea maombi yake kwa Bikira Maria na kuomba baraka zake na kutoka kwa Bwana kwa ajili ya safari ya Poland na kwa ajili ya adhimisho ya Siku ya Vijana Duniani.
Na mapema Jumatano hii, kabla ya safari akiwa Vatican alikwenda katika Kaburi la Mtakatifu Yohane Paulo II, kuomba maombezi yake yamsindikize. Na wakati akiondoka katika makazi yake ya Jengo la Mtakatifu Marta, aliangana na kikundi cha vijana wakimbizi wapato 15 tisa wakiwa wavulana na sita wasichana kutoka mataifa mbalimbali , ambao wameingia hapa Roma na bado hawana hati za kuwawezesha kusafiri nje ya Italia. Vijana hao wanaopata msaada wa kuishi katika jengo la Kipapa, walimtakia Papa safari njema na maadhmisho mema ya Siku ya V ijana ya Dunia , ambayo wao hawawezi kwenda kushiriki moja kwa moja lakini wakaahidi kwamba watakuwa pamoja nae kiroho.
Papa atakuwa Poland hadi siku ya Jumapili tarehe 31 Julai, na ratiba yake kwa kifupi ni kama ifuatavyo:
Jumatano 27.Julai majira ya saa kumi na moja atakutana na Utawala wa Poland katika ukumbi wa Wawel Krakow na baada ye majira ya saa kumi na mbili na nusu atakutana ma Maaskofu wa Poland katika Kanisa Kuu la Krakow.
Alhamis28: majira ya saa nne ataongoza Ibada ya Misa katiak Madhabahu ya Jasna Gora ya Czestochowa Na saa kumi na moja na nusu za jioni , atapokewa rasmi katika Mkutano uwanja wa Jordan wa Krakow.
Ijumaa 29 Julai:majira ya saa kumi na nusu za jioni atatembelea hospital ya watoto ya Prokocim Krakow, baada ye kuongoza Ibada ya Njia ya Msalba huko Spianata Blonia.
Jumamosi 30: majira ya saa tatu na nusu ataongoza Ibada ya Misa kwa ajili ya Mapadre, Watawa , walioweka maisha wakfu na waseminaristi katika Madhabahu ya Yohana Paulo 11. Na saa moja na nusu za jioni kushiriki katika mkesha wa maombi akiwa na vijana
Jumapili majira ya saa nne ataongoza maadhmisho ya Ibada ya Misa kwa ajili ya Siku ya Vijana ya Dunia ya 31 na baadaye sala ya Malaika wa Bwana na kukutana na vijana wa kujitolea majira ya saa kumi na moja za jioni. Na kunako saa kumi na mbili za jioni ataanza safari ya kureje Roma , kwa ndege namba LOT /B787 hadi uwanja wa fiumicino Roma.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni