0
SOMO 1
Hek 18: 6-9

Usiku ule baba zetu walitangulia kuonywa, ili wakiwa na ufahamu hakika, wafurahishwe na viapo walivyovitegemea; kwa hiyo watu wako waliutazamia wokovu wa wenye haki na uharibifu wa adui. Madhali uliwalipia kisasi watesi wale, na kwa njia ile ile uliwatukuza ukituita ili tukujie. Zaidi ya hayo watoto watakatifu wa watu wema walitoa dhabihu kwa siri, na kwa moyo mmoja walijitwalia agano la torati ya dini, ya kwamba watashirikiana katika mambo mema na vile vile katika hatari; pindi walipoimbisha nyimbo takatifu za mababu katika kumhimidi Mungu.

Neno la Mungu...Tumshukuru Mungu


WIMBO WA KATIKATI 
Zab. 33 :1, 12, 18-16,20-22 (K) 12

(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.

Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, 
Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Watu aliowachagua kuwa urithi wake. (K) 

Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao, 
Wazingojea fadhili zake.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa. (K)

Nafsi zetu zinamngoja Bwana,
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivvokungoja Wewe. (K)


SOMO 2 
Ebr 11: 1-2, 8-19

Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Maana Ibrahimu aiipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa ugenlni katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.

Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji. Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; Naam. yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.

Neno la Mungu...Tumshukuru Mungu


SHANGILIO 
Yn. 8: 12

Aleluya, aleluya, 
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu. asema Bwana: Yeye anifuataye atakuwa na nuru ya uzima.
 Aleluya.


INJILI 
Lk. 12: 32-48

Yesu aliwaambia makutano: Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme. Viuzeni mlivyo navvo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa. akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu. Kwa kuwa hazina yenu ilipo, ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu.

Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; nanyi iweni kama watu wanaomng jea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwa- karibisha chakulani, atakuja na kuwahudumia. Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwa kuta hivi, heri watumwa hao. Lakini fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi; angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.

Petro akamwambia, Bwana, mithali hiyo umetuambia sisi tu, au watu wote pia? Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, arnbaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, arnbaye bwana wake ajapo atamkuta anafanva hivyo. Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini. Na mtumwa yule aliye  jua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. Na yule asiyejua, nave amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.

Chapisha Maoni

 
Top