(Vatican Radio) Jumatatu hii majira ya saa nne za asubuhi, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Jimbo Takatifu ,aliongoza Maadhimisho ya Misa ya Shukurani , kwa ajili ya Mama Tereza wa Calcutta kutangazwa Mtakatifu na Papa Francisko Jumapili iliyopita
Katika homilia yake, Kardinali Parolin alikumbuka mambo kadhaa muhimu katika maisha ya Mtakatifu Mama Tereza, hasa kiu yake kwa Mungu, kiu iliyoongoza kila hatua ya utendaji wake. 'Caritas Christi urget nos”: " Upendo wa Kristo" unaotuchochea sisi sote , yalikuwa ni maneno yaliyorudiwa mara kwa mara na Kardinali Parolini katika mahubiri yake, kwenye ibada hii ya Misa ya Shukurani.
Alisema , maneno haya, yanaonyesha moto wote wa upendo uliomvutia yule tunayemtaja sasa kuwa Mtakatifu Mama Tereza wa Calcutta , ambaye anatupa mfano wa maisha ya upendo kwa jirani , mfano tunaotakiwa kwa sisi sote kuufuata. Kardinali Parolini aliendelea kuyatafakari maisha ya Mtakatifu Mama Tereza akisema ni maisha yanayoweza kufananishwa na 'kalamu ndogo katika mikono ya Mungu'.
Aidha alimtaja Mtakatifu Mama Teresa, kuwa sawa na kioo wazi kinachoonyesha upendo wa Mungu katika uhusiano wetu na majirani zetu , hasa kwa watu maskini zaidi walio telekezwa miitani kama ilivyo kwa watu wa kabila la Wadelit wa India. Aidha alikumbuka mahangaiko na changamoto zilizomkabili mara kwa mara ya Mama Tereza kwa ajili ya kutetea haki za wasiozaliwa bado, ambao aliwatambua kuwa kundi la watu wanyonge maskini wa maskini wasioweza kujitetea kwa lolote, watu waliojisikia kutopendwa , kwa unyonge wao walionekama kama hawana maana bali ni waktu wa kupuuzwa tu.
Mama Tereza kwa utambuzi huu aliweza leta mwamko mpya wa kutambuliwa kwa haki na thamani hata ya mtu asiyezaliwa bado , mtoto aliye tumboni mwa mamaye , anayetishwa na ”umaskini wa maskini". Kwa Mama Tereza kila mmoja wao , hutegemea zaidi ya yote, upendo na huduma ya kimama na ulinzi wa jamii.
Kardinali Parolin pia alikumbuka tukio jingine la kihistoria ambamo Mama Teresa aliteuliwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya mwaka 1979, ambamo katika hotuba yake alisema, ni muhimu sana kutambua kwamba , upendo wa kweli huumiza, kama Yesu alivyoteseka kwa kutupenda. Kardinali amesema, maneno haya yanaonyesha mlango wa kuingia katika maisha Mtakatifu, ni lazima kupita katika dibwi la mateso kwa ajili ya wengine.
Kardinali Parolin alihitimisha homilia yake kwa kukumbuka maneno mawili yaliyotundikwa katika kila nyumba ya Watawa Wamisionari wa Upendo: 'Naona kiu.
'Naona kiu, amesema 'kiu ya maji safi, kiu kwa ajili ya nafsi zinazo hitaji kufarijiwa na kukombolewa kutoka maisha maovu m kiu y kuwafanya wazuri wa kupendeza mbele ya kupendeza machoni ya Mungu, kiu kwa Mungu, kiu kwa muhimu wake na ung’avu wa uwepo wake. Naona kiu: ; hii ni kiu iliyouchoma moyo wa Mama Teresa:Msalaba wake na furaha zake , mateso yake na utukufu wake .
Mtakatifu Mama Tereza utuombee
Wakati wa Ibada ya kumtangaza kuwa Mtakatifu , Masalia ya Mtakatifu Mama Tereza , yaliwekwa katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu , ambayo ni kipande kidogo cha mtandio wake uliokuwa na madoa ya damu yake. Masalia hayo Jumatatu hii yameweka katika Kanisa Kuu la Yohane wa Laterano , ambako kulifanyika Ibada ya kumtaja kuwa Mwenyeheri
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni