Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Augustine Kasujja kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Luxembourg na wakati huo huo, ataendelea kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ubelgiji! Askofu mkuu Kassuja alizaliwa kunako tarehe 26 Aprili 1946 huko Mitala- Maria nchini Uganda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 6 Januari 1973. Tarehe 26 Mei 1998 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Balozi wa kwanza kutoka Afrika na kumtumwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Algeria na Tunisia.
Tarehe 22 Agosti 1998 akawekwa wakfu. Kunako tarehe 22 Aprili 2004 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Madagascar, Visiwa vya Usheli sheli, Comoro na Mauritius. Tarehe 2 Februari 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteua kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Nigeria. Tarehe 12 Oktoba 2016 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ubelgiji na mwishoni tarehe 7 Desemba 2016 ameteuliwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Luxembourg.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni