0

Hivi karibuni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu huko Abu Dhambi nchini Uarabuni, ilifanyika maadhimisho ya kihistoria. Ilikuwa ni maadhimisho ya miaka 100 ya uwepo wa Ndugu wafransiskani Wakapuchini kutoka Mkoa wa  Toscan nchini Italia katika Vikarieti ya kitume nchi za uarabuni.
Kwenye maadhimisho hayo alikuwepo Padre Angelo Fiumicelli mwenye umri wa miaka 91 ambaye amekuwa mmoja wa mmisioanari walioko nchi za uarabuni lakini kwa miaka ya hivi karibuni amerudi nchini Italia; Padre Eugenio Mattioli 86 bado yuko katika utume wa kimisionari na  viongozi mbalimbali  wa dini kama vile Monsinyo Paul Hinder Vika wa kitume nchi ya Uarabuni Kusini; Balozi wa kitume wa Papa Askofu Mkuu Francisco Padilla, Mkuu wa Shirika wa Wakapunchini Padre Mauro Jöhri; na Mkuu wa wakapuchini kanda ya Toscana Padre Valerio Mauro. Wengine ni mapadre 43 kutoka katika maparokia ya vikarieti ya nchi za
uarabuni  na karibia waamiini 200,000.
Tangu mwanzo wa utume wa ndugu wadogo wakapuchini ulikuwa mgumu na mwaka 1888 waliazna kufungua mashule na kujenga makanisa huko Aden na pia nyumba ya vikarieti Vilevile  hata karibu katika nchi za uarabuni mwaka 1916. Hiyo yote iliwezekana kutokana na ukarimu , mshikamano  na msaada wa mashehe, walio toa maeneo yao kuwezesha ujenzi wa maeneo matakatifu.
Kwa namna hiyo makanisa yamejengwa ya Bahrain 1939 na karibia katika nchi za Umoja wa nchi za Urabuni na Oman mwaka 1960. Hata juhudi  zaidi za utume zilifanywa na Monsinyo Berdardo Gremoli , msimamizi wa kitume wa Papa tangu 1976 hadi 2005. Kanisa mahalia liko ndani ya wakazi wa kiislam;ambapo kuna zaidi ya milioni moja ya wabatizwa na sehemu kubwa  wanatumia  liturujia za nchi za mashariki, kama vile maronite, melkite, Kiarmenia, syria, Syiria malabar , na syria-Malankara.
Pamoja na kutumia lugha ya Kingreza na Kiaraba katika maadhimisho yao pia wanatumia lugha ya Kimalayalamu, Konkani, Kitagalogi, Kifaransa, Kiitaliano, Kijerumani, Kisinhali na Tamil. Hayo yamesema na Balozi wa kitume wa nchi za uarabuni na kwamba  katika maeneo hayo siku ya mapunziko ni Ijumaa, kwa namna siiyo maadhimishi ya ibada ya misa jumapili tu bali hata alhamisi na Ijumaa jioni. Anaongeza;hizi ibada ni maarufu zaidi na kila wiki watu hukusanyika katika Makanisa na umati huo ni kusema kwamba hata Kuhani yoyote wa nchi za Ulaya angeota.
Maneno hayo yanadhihilishwa kwani maparokia 16 yaliyopo  katika vikarieti , inawashirikisha wastani wa 2,700 ya wabatizwa kwa mwaka. 30,342 ni vijana wanoudhulia katekisimu;268 ndoa na 21,047 ni vijana na kati yao 3,637 ni wakatoliki wanao kwenda katika shule zinazoendeshwa na watawa.
Sr Angela rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

Chapisha Maoni

 
Top