I. MTAGUSO WA KWANZA WA NICEA (Mwaka
325)
Muhtasari: Mtaguso
wa Nicea ulifanyika kwa miezi miwili na siku kumi na mbili. Ulihusisha maaskofu
380. Mkutano huo ulisimamiwa na Hosius, Askofu wa Cordova. Huyu ndiye
aliyemwakilisha Baba Mtakatifu wa enzi hizo Sylvester. Mfalme Konstantino
alihudhuria pia. Kutokana na mtaguso huu tumepata kanuni ya imani ile fupi
ijulikanayo kama kanuni ya imani ya Nicea. Mtaguso uliyapinga mafundisho ya
Arius na hivyo kusisitiza umungu kweli wa Mwana wa Mungu yaani Yesu Kristo
ukisema kwamba Mungu Mwana ana hali ileile ya Baba (homoousios). Halafu mtaguso
uliamua utaratibu wa kupata tarehe ya kuadhimisha Pasaka kila mwaka (yaani
kabla au baada kidogo ya ekwinoksi ya mwezi Machi). Tarehe hiyo iliwekwa
kuwajibu wazushi fulani, wazushi waliojulikana kwa jina la Wakwatodesimani)
.
II. MTAGUSO WA
KWANZA WA KONSTANTINOPLE (LEO INSTANBUL - Mwaka 381)
Muhtasari: Mtaguso
wa kwanza wa Konstantinople ulifanyika chini ya usimamizi wa Baba Mtakatifu
Damaso na Mfalme Theodosius I. Maaskofu 150 walihudhuria. Mtaguso ulikuwa dhidi
ya wafuasi wa Macedonius aliyepinga umungu wa Roho Mtakatifu. Ndipo zikaongezwa
kwenye kanuni ya imani ya Nicea kweli kadhaa kumhusu Roho Mtakatifu (ndiyo
maana sehemu ile inayomhusu Roho Mtakatifu imepanuka. Kweli zilizoongezwa ni
hizo kuanzia: “anayeabudiwa na kutukuzwa sawa na Baba na Mwana” na kuendelea
mpaka mwishoni.
III. MTAGUSO WA
EFESO (Mwaka: 431)
Muhtasari: Mtaguso
wa Efeso uliongozwa na Mt. Cyril wa Alexandria akimwakilisha Baba Mtakatifu
Selestine. Maaskofu zaidi ya 200 walihudhuria. Mtaguso ulithibitisha umoja wa
nafsi ya Yesu, ukamtangaza Maria kuwa Mama wa Mungu (theotokos) dhidi ya
Nestorius, Askofu wa Konstantinople aliyekataa umama wa Mungu wa Maria na
ukarudia kuyalaani mafundisho ya kizushi ya Pelagius aliyefundisha ovyo kuhusu
neema na maongozi ya
Mungu
IV. MTAGUSO WA
KALSEDONI (Mwaka: 451)
Muhtasari: Mtaguso
wa Kalsedoni uliongozwa na Baba Mtakatifu Leo Mkuu na Mfalme Marsiani. Maaskofu
150 walihudhuria. Uthibithisha hali mbili katika Yesu Kristo yaani hali ya
kimungu na hali ya kibinadamu dhidi ya Eutyches aliyefundisha kinyume na ukweli
huo.
Eutyches alitengwa na mtaguso huo
V. MTAGUSO WA PILI
WA KONSTANTINOPLE (Mwaka: 553)
Muhtasari: Mtaguso
wa pili wa Konstantinople uliongozwa na Baba Mtakatifu Vigilius na Mfalme
Yustiani I. Maaskofu 165 walihudhuria. Mtaguso ulilaani mafundisho ya kizushi
ya Orijeni na maandishi fulani (Sura Tatu) ya Theodoret, na mafundisho ya
Theodore, Askofu wa Mopsuestia pamoja naya Ibas, Askofu wa Edessa. Mtaguso huu
ulithibitisha mitaguso minne iliyotangulia hususani ule wa Kalsedoni. Ikumbukwe
maamuzi ya mtaguso wa Kalsedoni yalikuwa yanapingwa na wazushi kadhaa
VI. MTAGUSO WA TATU
WA KONSTANTINOPLE (Mwaka: 680-681)
Muhtasari: Mtaguso
wa Tatu wa Konstantinople uliongozwa na Baba Mtakatifu Agatho na Mfalme
Konstantine Pogonatus. Ulihudhuriwa na Maaskofu (Mapatriaki) wa Konstantinople
na wa Antiokia pamoja na maaskofu 174. Mtaguso ulikomesha mafundisho ya uzushi
kwamba Yesu ana utashi mmoja tu (Monothelitism) ukasema kwamba Yesu ana tashi
mbili, yaani utashi wa kimungu na utashi wa kibinadamu. Ulisema kwamba tashi
hizo mbili ndizo zilihusika katika utendaji wake. Ndipo ukawapiga marufuku
akina Sergius, Pyrrhus, Paul, Macarius pamoja na wafuasi wao wote
.
VII. MTAGUSO WA PILI
WA NICEA (Mwaka: 787)
Muhtasari: Mtaguso
wa Pili wa Nicea uliitishwa na Mfalme Konstantine VI na mama yake Irene.
Mtaguso uliongozwa na Baba Mtakatifu Adrian I chini ya uenyekiti wa wawakilishi
wa Baba Mtakatifu Adrian. Maaskofu kati ya 300 na 367 walihudhuria. Mtaguso
uliratibisha vyema mafundisho juu ya heshima kwa picha takatifu. Mtaguso huu
ulifuatia wimbi la kuharibu picha na sanamu lililoletwa na wapinga sanamu
(iconoclast)
VIII. MTAGUSO WA NNE
WA KONSTANTINOPLE (Mwaka: 869)
Muhtasari: Mtaguso
wa Nne wa Konstantinople uliongozwa na Baba Mtakatifu Adriani II na Mfalme
Basili. Maaskofu 102, wawakilishi wa Baba Mtakatifu watatu, na maaskofu wa
Mashariki (mapatriaka) wanne walihudhuria. Mtaguso ulichoma hati na maandishi
yaliyotoka kwenye mtaguso batili (conciliabulum) ulioitishwa na Photius
kuwapinga Baba Mtakatifu Nicholas na Ignatius aliyekuwa Askofu (Patriaka)
halali wa Konstantinople. Mtaguso huo ulimkataa Photius aliyejinyakulia pasipo
halali hadhi ya uaskofu (upatriaka). Hata hivyo Mtengano wa Photiani ulishika
hatamu katika katika Kanisa la Kigiriki. Na tangu wakati huo hadi leo hii
hakujaitishwa mtaguso wowote huko Mashariki.
IX. MTAGUSO WA
KWANZA WA LATERANI (Mwaka: 1123)
Muhtasari: Mtaguso
wa Kwanza wa Laterani ndiyo mtaguso wa kwanza kufanyika mjini Roma. Uliitishwa
na Baba Mtakatifu Callistus II. Maaskofu na maabate 900 walihudhuria. Mtaguso
huu ulifuta haki iliyodaiwa na watawala walei kujivisha pete na misalaba na
kujimilikisha mali za Kanisa. Mtaguso ulishughulikia pia nidhamu ya Kanisa na
vita za kuikomboa Nchi Takatifu kutoka mikononi mwa makafiri (yaani watu wasio
Wakristo). Maamuzi haya yalitoa ruhusa kuanza kwa vita vya msalaba (crusades).
X. MTAGUSO WA PILI
WA LATERANI (Mwaka 1139)
Muhtasari: Mtaguso
wa Pili wa Laterani ulifanyika Roma ukiongozwa na Baba Mtakatifu Innosenti II.
Takribani maskofu 1000 pamoja na Mfalme Konradi walihudhuria. Mtaguso
ulikusudia kukomesha mafundisho ya uongo ya Arnold wa Brescia.
XI. MTAGUSO WA TATU
WA LATERANI (Mwaka 1179)
Muhtasari: Mtaguso
wa Tatu wa Laterani uliitishwa na Baba Mtakatifu Alexander III wakati ule
Frederick I alipokuwa mfalme. Maaskofu 302 walihudhuria. Mtaguso ulilaani
mafundisho ya kizushi ya Waalbigensi na Waldensi na ulitoa dikrii kadhaa za
kurekebisha maadili
XII. MTAGUSO WA NNE
WA LATERANI (Mwaka 1215)
Muhtasari: Mtaguso
wanne wa Laterani uliongozwa na Baba Mtakatifu Innocent III. Mapatriaka wa
Konstantinople na Yerusalemu, maaskofu wakuu 71, maaskofu wa kawaida 412,
maabate 800 na viongozi wakuu (maprimate) wa Wamaroniti pamoja na Mtakatifu
Dominiko walihudhuria. Mtaguso ulitoa kanuni ya imani kubwa dhidi ya
Waalbigensi (Firmiter credimus).Nao ulilaani mafundisho ya uongo juu ya Abate
Yoakim juu ya Utatu Mtakatifu. Tena ulitoa dikrii sabini za marekebisho.
Mtaguso huu ndio mtaguso muhimu zaidi wa miaka ile ya kati nao ulikuwa kilele cha
maisha ya Kanisa na nguvu za Baba Mtakatifu
XIII. MTAGUSO WA
KWANZA WA LYON (Mwaka 1245)
Muhtasari: Mtaguso
wa Kwanza wa Lyon uliongozwa na Baba Mtakatifu Innocent IV. Mapatriaka wa
Konstantinople, Antiokia na Aquileia (Venice), maaskofu 140, Mfalme Baldwin II
Mfalme wa Mashariki pamoja na Mt. Louis aliyekuwa Mfalme wa Ufaransa
walihudhuria. Mtaguso ulipitisha maamuzi ya kumtenga na kumwondosha madarakani
Mfalme Frederick II na ukaamrisha vita vipya vya msalaba majeshi yake
yakiongozwa na Mt. Louis. Vita hivi vipya vilipiganwa dhidi ya Wasaraseni na
Wamongoli.
XIV. MTAGUSO WA PILI
WA LYON (Mwaka 1274)
Muhtasari: Mtaguso
wa Pili wa Lyon uliongozwa na Baba Mtakatifu Gregory X. Mapatriaka wa Antiokia
na Konstantinople, makardinali 15, maaskofu 500 na waheshimiwa wengine zaidi ya
1000 walihudhuria. Mtaguso huu uliwezesha muungano wa muda wa Kanisa la
Kigiriki na Kanisa la Roma. Katika mtaguso huu maneno “na Mwana” (filioque)
yaliongezwa kwenye kanuni ya imani ile ya Konstantinople na hivyo kuwa “atokaye
kwa Baba na Mwana”. Mtaguso huu ulitafuta namna ya kuikomboa nchi ya Palestina
kutoka katika mikono ya Waturuki. Pia uliratibu kanuni za uchaguzi wa Baba
Mtakatifu.
XV. MTAGUSO WA
VIENNE (Mwaka: 1311-1313)
Muhtasari: Mtaguso
wa Vienne ulifanyika katika mji huo wa Ufaransa kwa amri ya Baba Mtakatifu
Klementi V, aliyekuwa Baba Mtakatifu wa kwanza kati ya Mababa watakatifu
waliokaa Avignon. Mapatriaka wa Antiokia na Alexandria, maaskofu 300 (lakini
kumbukumbu zingine husema walikuwa 114), na wafalme watatu, yaani Mfalme Filipo
IV wa Ufaransa, Mfalme Edward II wa Uingereza na Mfalme James II wa Aragon
walihudhuria. Mtaguso huu ulishughulikia makosa na mafundisho ya uongo ya
makundi yafuatayo: Watempla, Waraticheli, Wabeghardi na Wabeguini.
Ulishughulikia pia kupanga vita mpya ya msalaba, marekebisho ya makleri na
ufundishaji wa lugha za nchi za Mashariki katika vyuo vikuu.
XVI. MTAGUSO WA
KONSTANSI (Mwaka: 1414-1418)
Muhtasari: Mtaguso
wa Konstansi ulifanyika wakati wa mgawinyiko mkuu wa Magharibi. Mtaguso huu
ulikusudia kumaliza migawanyiko katika Kanisa. Lakini mtaguso huo ulipata
uhalali pale Baba Mtakatifu Gregory XI alipouitisha rasmi. Kwa hali hii
ulifanikiwa kusitisha mgawanyiko kwa kumchagua Baba Mtakatifu Martin V. Mtaguso
wa Pisa (mwaka 1403) ulishindwa kufanya jambo hili kwa sababu ya uharamu wake.
Basi, Baba Mtakatifu halali alithibitisha dikrii za sinodi ya awali dhidi ya
Wyclif na Hus. Mtaguso huu ulijipatia hadhi ya kiuekumene katika vikao vyake
vya mwishoni yaani vikao vya 42 hadi 45 na vile vile kwa kuthibitishwa kwa
dikrii zake za mwanzo na Baba Mtakatifu Martin V.
XVII. MTAGUSO WA
BASLE/FERRARA/FLORENCE (Mwaka: 1431-1439)
Muhtasari: Mtaguso
wa Basle ulifanyika kwanza katika mji huu. Wakati huo Baba Mtakatifu alikuwa
Eugene IV na Sigismund alikuwa mfalme wa Dola ya Rumi. Mtaguso huo ulikusudia
kuleta upatanisho wa kidini kwa Bohemia. Baada ya kuzuka ugomvi dhidi ya Baba
Mtakatifu mtaguso ulihamishiwa Ferrara (1438),na kishapo Florence (1439), ambapo
muungano uliodumu kwa muda mfupi na Kanisa la Kigiriki ulifikiwa, Wagiriki
wakipokea maamuzi ya mtaguso mintarafu masuala yaliyokuwa yakibishaniwa.
Mtaguso wa Basle ulikuwa wa kiuekumene hadi kikao cha ishirini na tano, na Baba
Mtakatifu Eugene IV alithibitisha dikrii zile tu zilizohusika na kumaliza
mafundisho ya kizushi, amani ya Ukristo, marekebisho ya Kanisa wakati huo huo
zisizoharibu haki za Kiti cha Baba Mtakatifu.
XVIII. MTAGUSO WA
TANO WA LATERANI (Mwaka: 1512-1517)
Muhtasari: Mtaguso
wa Tano wa Laterani ulifanyika tangu 1512 hadi 1517. Mababa watakatifu Julius
II na Leo X, waliongoza mtaguso huu wakati ule mfalme akiwa Maximilian I.
Makardinali 15 na takribani maaskofu wakuu na maaskofu wa kawaida 80
walihudhuria. Kimsingi dikrii zake zinahusu nidhamu. Vita vipya vya msalaba
dhidi ya Waturuki vilipangwa lakini havikufanyika kutokana na mgogoro wa kidini
uliotokea huko Ujerumani uliosababishwa na Martin Luther.
XIX. MTAGUSO WA
TRENTO (Mwaka: 1545-1563)
Muhtasari: Mtaguso
wa Trento ulichukua miaka kumi na minane (1545-1563). Mtaguso huu uliendeshwa
na Mababa watakatifu watano: Paul III, Julius III, Marcellus II, Paul IV na
Pius IV, katika enzi za wafalme Charles V na Ferdinand. Makardinali 5
wawakilishi wa Kiti cha Baba Mtakatifu. Mapatriaka 3, maaskofu wakuu 33,
maaskofu 235, maabate 7, wakuu wa mashirika 7 na wataalamu wa teolojia 160
walihudhuria. Mtaguso uliitishwa kuchunguza na kulaani makosa yaliyotangazwa na
Martin Luther na Wanamageuzi pamoja na kurekebisha nidhamu ya Kanisa. Kati ya
mitaguso yote huu ndio mtaguso uliochukua muda mrefu sana nao ulitoa dikrii
nyingi sana za kidogma na za marekebisho na ulitoa mapato yenye faida sana.
XX. MTAGUSO WA
KWANZA WA VATIKANO (Mwaka: 1869-1870)
Muhtasari: Mtaguso
wa Kwanza wa Vatikano uliitishwa na Baba Mtakatifu Pius IX. Mtaguso ulianza 8
Desemba, 1869 na kughairishwa 18 Julai, 1870; mpaka mwaka 1908 ulikuwa
haujamalizika. Watu 803 walihudhuria kwa mgawanyiko ufuatao: maaskofu wa kiwana
mfalme 6, makardinali 49, mapatriaka 11, maaskofu wakuu na maaskofu 680,
maabate 28 na wakuu wa mashirika 29.Mbali ya maamuzi muhimu kuhusu imani na
muundo wa Kanisa, mtaguso huu ulitangaza kutokukosea kwa Baba Mtakatifu
akitangaza kitu kutoka kwenye kiti chake cha upapa (ex cathedra), yaani kama
mchungaji na mwalimu wa Wakristo wote akitangaza fundisho la imani lenye
kuhusiana na imani au maadili linalokusudiwa kushikwa na Kanisa zima.
XXI. MTAGUSO WA PILI
WA VATIKANO (Mwaka: 1962-1965)
Muhtasari: Mtaguso
huu uliitishwa na Baba Mtakatifu Yohane XXIII na kumalizwa na Baba Mtakatifu
Paulo VI. Viongozi 2860 walihudhuria. Lengo kuu la mtaguso huu lilikuwa
kuchunguza na kubainisha wazi nafasi ya Kanisa ulimwenguni, uekumene, upyaisho
wa maisha ya wakfu (kitawa), maisha na utume wa mapadre na nafasi ya walei kama
wadau wa uinjilishaji wa ulimwengu. Yalichunguzwa maboresho ya liturujia.
Mtaguso ulipendekeza Misa iadhimishwe katika lugha mbalimbali badala ya
Kilatini. Mafundisho ya Mtaguso wa Vatikano II yamo katika hati 16: konstitusio
4, dikrii 9 na matamko 3.
Mmeniuliza swali
niwapatie orodha ya mitaguso ya kiukumene iliyopata kufanyika na muhtasari wa
mambo makuu yaliyojadiliwa. Basi, ifuatayo ndiyo orodha yenyewe.
I. MTAGUSO WA KWANZA
WA NICEA (Mwaka 325)
Muhtasari: Mtaguso
wa Nicea ulifanyika kwa miezi miwili na siku kumi na mbili. Ulihusisha maaskofu
380. Mkutano huo ulisimamiwa na Hosius, Askofu wa Cordova. Huyu ndiye
aliyemwakilisha Baba Mtakatifu wa enzi hizo Sylvester. Mfalme Konstantino
alihudhuria pia. Kutokana na mtaguso huu tumepata kanuni ya imani ile fupi
ijulikanayo kama kanuni ya imani ya Nicea. Mtaguso uliyapinga mafundisho ya
Arius na hivyo kusisitiza umungu kweli wa Mwana wa Mungu yaani Yesu Kristo
ukisema kwamba Mungu Mwana ana hali ileile ya Baba (homoousios). Halafu mtaguso
uliamua utaratibu wa kupata tarehe ya kuadhimisha Pasaka kila mwaka (yaani
kabla au baada kidogo ya ekwinoksi ya mwezi Machi). Tarehe hiyo iliwekwa
kuwajibu wazushi fulani, wazushi waliojulikana kwa jina la Wakwatodesimani).
II. MTAGUSO WA
KWANZA WA KONSTANTINOPLE (LEO INSTANBUL - Mwaka 381)
Muhtasari: Mtaguso
wa kwanza wa Konstantinople ulifanyika chini ya usimamizi wa Baba Mtakatifu
Damaso na Mfalme Theodosius I. Maaskofu 150 walihudhuria. Mtaguso ulikuwa dhidi
ya wafuasi wa Macedonius aliyepinga umungu wa Roho Mtakatifu. Ndipo zikaongezwa
kwenye kanuni ya imani ya Nicea kweli kadhaa kumhusu Roho Mtakatifu (ndiyo
maana sehemu ile inayomhusu Roho Mtakatifu imepanuka. Kweli zilizoongezwa ni
hizo kuanzia: “anayeabudiwa na kutukuzwa sawa na Baba na Mwana” na kuendelea
mpaka mwishoni.
III. MTAGUSO WA
EFESO (Mwaka: 431)
Muhtasari: Mtaguso
wa Efeso uliongozwa na Mt. Cyril wa Alexandria akimwakilisha Baba Mtakatifu
Selestine. Maaskofu zaidi ya 200 walihudhuria. Mtaguso ulithibitisha umoja wa
nafsi ya Yesu, ukamtangaza Maria kuwa Mama wa Mungu (theotokos) dhidi ya
Nestorius, Askofu wa Konstantinople aliyekataa umama wa Mungu wa Maria na
ukarudia kuyalaani mafundisho ya kizushi ya Pelagius aliyefundisha ovyo kuhusu
neema na maongozi ya Mungu
IV. MTAGUSO WA
KALSEDONI (Mwaka: 451)
Muhtasari: Mtaguso
wa Kalsedoni uliongozwa na Baba Mtakatifu Leo Mkuu na Mfalme Marsiani. Maaskofu
150 walihudhuria. Uthibithisha hali mbili katika Yesu Kristo yaani hali ya
kimungu na hali ya kibinadamu dhidi ya Eutyches aliyefundisha kinyume na ukweli
huo. Eutyches alitengwa na mtaguso huo
V. MTAGUSO WA PILI
WA KONSTANTINOPLE (Mwaka: 553)
Muhtasari: Mtaguso
wa pili wa Konstantinople uliongozwa na Baba Mtakatifu Vigilius na Mfalme
Yustiani I. Maaskofu 165 walihudhuria. Mtaguso ulilaani mafundisho ya kizushi
ya Orijeni na maandishi fulani (Sura Tatu) ya Theodoret, na mafundisho ya
Theodore, Askofu wa Mopsuestia pamoja naya Ibas, Askofu wa Edessa. Mtaguso huu
ulithibitisha mitaguso minne iliyotangulia hususani ule wa Kalsedoni. Ikumbukwe
maamuzi ya mtaguso wa Kalsedoni yalikuwa yanapingwa na wazushi kadhaa
VI. MTAGUSO WA TATU
WA KONSTANTINOPLE (Mwaka: 680-681)
Muhtasari: Mtaguso
wa Tatu wa Konstantinople uliongozwa na Baba Mtakatifu Agatho na Mfalme
Konstantine Pogonatus. Ulihudhuriwa na Maaskofu (Mapatriaki) wa Konstantinople
na wa Antiokia pamoja na maaskofu 174. Mtaguso ulikomesha mafundisho ya uzushi
kwamba Yesu ana utashi mmoja tu (Monothelitism) ukasema kwamba Yesu ana tashi
mbili, yaani utashi wa kimungu na utashi wa kibinadamu. Ulisema kwamba tashi
hizo mbili ndizo zilihusika katika utendaji wake. Ndipo ukawapiga marufuku
akina Sergius, Pyrrhus, Paul, Macarius pamoja na wafuasi wao wote.
VII. MTAGUSO WA PILI
WA NICEA (Mwaka: 787)
Muhtasari: Mtaguso
wa Pili wa Nicea uliitishwa na Mfalme Konstantine VI na mama yake Irene.
Mtaguso uliongozwa na Baba Mtakatifu Adrian I chini ya uenyekiti wa wawakilishi
wa Baba Mtakatifu Adrian. Maaskofu kati ya 300 na 367 walihudhuria. Mtaguso
uliratibisha vyema mafundisho juu ya heshima kwa picha takatifu. Mtaguso huu
ulifuatia wimbi la kuharibu picha na sanamu lililoletwa na wapinga sanamu
(iconoclast)
VIII. MTAGUSO WA NNE
WA KONSTANTINOPLE (Mwaka: 869)
Muhtasari: Mtaguso
wa Nne wa Konstantinople uliongozwa na Baba Mtakatifu Adriani II na Mfalme
Basili. Maaskofu 102, wawakilishi wa Baba Mtakatifu watatu, na maaskofu wa
Mashariki (mapatriaka) wanne walihudhuria. Mtaguso ulichoma hati na maandishi
yaliyotoka kwenye mtaguso batili (conciliabulum) ulioitishwa na Photius
kuwapinga Baba Mtakatifu Nicholas na Ignatius aliyekuwa Askofu (Patriaka)
halali wa Konstantinople. Mtaguso huo ulimkataa Photius aliyejinyakulia pasipo
halali hadhi ya uaskofu (upatriaka). Hata hivyo Mtengano wa Photiani ulishika
hatamu katika katika Kanisa la Kigiriki. Na tangu wakati huo hadi leo hii
hakujaitishwa mtaguso wowote huko Mashariki.
IX. MTAGUSO WA
KWANZA WA LATERANI (Mwaka: 1123)
Muhtasari: Mtaguso
wa Kwanza wa Laterani ndiyo mtaguso wa kwanza kufanyika mjini Roma. Uliitishwa
na Baba Mtakatifu Callistus II. Maaskofu na maabate 900 walihudhuria. Mtaguso
huu ulifuta haki iliyodaiwa na watawala walei kujivisha pete na misalaba na
kujimilikisha mali za Kanisa. Mtaguso ulishughulikia pia nidhamu ya Kanisa na
vita za kuikomboa Nchi Takatifu kutoka mikononi mwa makafiri (yaani watu wasio
Wakristo). Maamuzi haya yalitoa ruhusa kuanza kwa vita vya msalaba (crusades)
.
X. MTAGUSO WA PILI
WA LATERANI (Mwaka 1139)
Muhtasari: Mtaguso
wa Pili wa Laterani ulifanyika Roma ukiongozwa na Baba Mtakatifu Innosenti II.
Takribani maskofu 1000 pamoja na Mfalme Konradi walihudhuria. Mtaguso
ulikusudia kukomesha mafundisho ya uongo ya Arnold wa Brescia.
XI. MTAGUSO WA TATU
WA LATERANI (Mwaka 1179)
Muhtasari: Mtaguso
wa Tatu wa Laterani uliitishwa na Baba Mtakatifu Alexander III wakati ule
Frederick I alipokuwa mfalme. Maaskofu 302 walihudhuria. Mtaguso ulilaani
mafundisho ya kizushi ya Waalbigensi na Waldensi na ulitoa dikrii kadhaa za
kurekebisha maadili
XII. MTAGUSO WA NNE
WA LATERANI (Mwaka 1215)
Muhtasari: Mtaguso
wanne wa Laterani uliongozwa na Baba Mtakatifu Innocent III. Mapatriaka wa
Konstantinople na Yerusalemu, maaskofu wakuu 71, maaskofu wa kawaida 412,
maabate 800 na viongozi wakuu (maprimate) wa Wamaroniti pamoja na Mtakatifu
Dominiko walihudhuria. Mtaguso ulitoa kanuni ya imani kubwa dhidi ya
Waalbigensi (Firmiter credimus).Nao ulilaani mafundisho ya uongo juu ya Abate
Yoakim juu ya Utatu Mtakatifu. Tena ulitoa dikrii sabini za marekebisho.
Mtaguso huu ndio mtaguso muhimu zaidi wa miaka ile ya kati nao ulikuwa kilele
cha maisha ya Kanisa na nguvu za Baba Mtakatifu
XIII. MTAGUSO WA
KWANZA WA LYON (Mwaka 1245)
Muhtasari: Mtaguso
wa Kwanza wa Lyon uliongozwa na Baba Mtakatifu Innocent IV. Mapatriaka wa
Konstantinople, Antiokia na Aquileia (Venice), maaskofu 140, Mfalme Baldwin II
Mfalme wa Mashariki pamoja na Mt. Louis aliyekuwa Mfalme wa Ufaransa
walihudhuria. Mtaguso ulipitisha maamuzi ya kumtenga na kumwondosha madarakani
Mfalme Frederick II na ukaamrisha vita vipya vya msalaba majeshi yake yakiongozwa
na Mt. Louis. Vita hivi vipya vilipiganwa dhidi ya Wasaraseni na Wamongoli.
XIV. MTAGUSO WA PILI
WA LYON (Mwaka 1274)
Muhtasari: Mtaguso
wa Pili wa Lyon uliongozwa na Baba Mtakatifu Gregory X. Mapatriaka wa Antiokia
na Konstantinople, makardinali 15, maaskofu 500 na waheshimiwa wengine zaidi ya
1000 walihudhuria. Mtaguso huu uliwezesha muungano wa muda wa Kanisa la
Kigiriki na Kanisa la Roma. Katika mtaguso huu maneno “na Mwana” (filioque)
yaliongezwa kwenye kanuni ya imani ile ya Konstantinople na hivyo kuwa “atokaye
kwa Baba na Mwana”. Mtaguso huu ulitafuta namna ya kuikomboa nchi ya Palestina
kutoka katika mikono ya Waturuki. Pia uliratibu kanuni za uchaguzi wa Baba
Mtakatifu.
XV. MTAGUSO WA
VIENNE (Mwaka: 1311-1313)
Muhtasari: Mtaguso
wa Vienne ulifanyika katika mji huo wa Ufaransa kwa amri ya Baba Mtakatifu
Klementi V, aliyekuwa Baba Mtakatifu wa kwanza kati ya Mababa watakatifu
waliokaa Avignon. Mapatriaka wa Antiokia na Alexandria, maaskofu 300 (lakini
kumbukumbu zingine husema walikuwa 114), na wafalme watatu, yaani Mfalme Filipo
IV wa Ufaransa, Mfalme Edward II wa Uingereza na Mfalme James II wa Aragon
walihudhuria. Mtaguso huu ulishughulikia makosa na mafundisho ya uongo ya
makundi yafuatayo: Watempla, Waraticheli, Wabeghardi na Wabeguini. Ulishughulikia
pia kupanga vita mpya ya msalaba, marekebisho ya makleri na ufundishaji wa
lugha za nchi za Mashariki katika vyuo vikuu.
XVI. MTAGUSO WA KONSTANSI (Mwaka: 1414-1418)
Muhtasari: Mtaguso
wa Konstansi ulifanyika wakati wa mgawinyiko mkuu wa Magharibi. Mtaguso huu
ulikusudia kumaliza migawanyiko katika Kanisa. Lakini mtaguso huo ulipata
uhalali pale Baba Mtakatifu Gregory XI alipouitisha rasmi. Kwa hali hii
ulifanikiwa kusitisha mgawanyiko kwa kumchagua Baba Mtakatifu Martin V. Mtaguso
wa Pisa (mwaka 1403) ulishindwa kufanya jambo hili kwa sababu ya uharamu wake.
Basi, Baba Mtakatifu halali alithibitisha dikrii za sinodi ya awali dhidi ya
Wyclif na Hus. Mtaguso huu ulijipatia hadhi ya kiuekumene katika vikao vyake
vya mwishoni yaani vikao vya 42 hadi 45 na vile vile kwa kuthibitishwa kwa
dikrii zake za mwanzo na Baba Mtakatifu Martin V.
XVII. MTAGUSO WA
BASLE/FERRARA/FLORENCE (Mwaka: 1431-1439)
Muhtasari: Mtaguso
wa Basle ulifanyika kwanza katika mji huu. Wakati huo Baba Mtakatifu alikuwa
Eugene IV na Sigismund alikuwa mfalme wa Dola ya Rumi. Mtaguso huo ulikusudia
kuleta upatanisho wa kidini kwa Bohemia. Baada ya kuzuka ugomvi dhidi ya Baba
Mtakatifu mtaguso ulihamishiwa Ferrara (1438),na kishapo Florence (1439),
ambapo muungano uliodumu kwa muda mfupi na Kanisa la Kigiriki ulifikiwa,
Wagiriki wakipokea maamuzi ya mtaguso mintarafu masuala yaliyokuwa
yakibishaniwa. Mtaguso wa Basle ulikuwa wa kiuekumene hadi kikao cha ishirini
na tano, na Baba Mtakatifu Eugene IV alithibitisha dikrii zile tu zilizohusika
na kumaliza mafundisho ya kizushi, amani ya Ukristo, marekebisho ya Kanisa
pasipo kuharibu haki za Kiti cha Baba Mtakatifu.
XVIII. MTAGUSO WA
TANO WA LATERANI (Mwaka: 1512-1517)
Muhtasari: Mtaguso
wa Tano wa Laterani ulifanyika tangu 1512 hadi 1517. Mababa watakatifu Julius
II na Leo X, waliongoza mtaguso huu wakati ule mfalme akiwa Maximilian I.
Makardinali 15 na takribani maaskofu wakuu na maaskofu wa kawaida 80
walihudhuria. Kimsingi dikrii zake zinahusu nidhamu. Vita vipya vya msalaba
dhidi ya Waturuki vilipangwa lakini havikufanyika kutokana na mgogoro wa kidini
uliotokea huko Ujerumani uliosababishwa na Martin Luther.
XIX. MTAGUSO WA
TRENTO (Mwaka: 1545-1563)
Muhtasari: Mtaguso
wa Trento ulichukua miaka kumi na minane (1545-1563). Mtaguso huu uliendeshwa
na Mababa watakatifu watano: Paul III, Julius III, Marcellus II, Paul IV na
Pius IV, katika enzi za wafalme Charles V na Ferdinand. Makardinali 5
wawakilishi wa Kiti cha Baba Mtakatifu. Mapatriaka 3, maaskofu wakuu 33,
maaskofu 235, maabate 7, wakuu wa mashirika 7 na wataalamu wa teolojia 160
walihudhuria. Mtaguso uliitishwa kuchunguza na kulaani makosa yaliyotangazwa na
Martin Luther na Wanamageuzi pamoja na kurekebisha nidhamu ya Kanisa. Kati ya
mitaguso yote huu ndio mtaguso uliochukua muda mrefu sana nao ulitoa dikrii
nyingi sana za kidogma na za marekebisho na ulitoa mapato yenye faida sana.
XX. MTAGUSO WA
KWANZA WA VATIKANO (Mwaka: 1869-1870)
Muhtasari: Mtaguso
wa Kwanza wa Vatikano uliitishwa na Baba Mtakatifu Pius IX. Mtaguso ulianza 8
Desemba, 1869 na kughairishwa 18 Julai, 1870; mpaka mwaka 1908 ulikuwa
haujamalizika. Watu 803 walihudhuria kwa mgawanyiko ufuatao: maaskofu wa kiwana
mfalme 6, makardinali 49, mapatriaka 11, maaskofu wakuu na maaskofu 680,
maabate 28 na wakuu wa mashirika 29.Mbali ya maamuzi muhimu kuhusu imani na
muundo wa Kanisa, mtaguso huu ulitangaza kutokukosea kwa Baba Mtakatifu
akitangaza kitu kutoka kwenye kiti chake cha upapa (ex cathedra), yaani kama
mchungaji na mwalimu wa Wakristo wote akitangaza fundisho la imani lenye
kuhusiana na imani au maadili linalokusudiwa kushikwa na Kanisa zima.
XXI. MTAGUSO WA PILI
WA VATIKANO (Mwaka: 1962-1965)
Muhtasari: Mtaguso
huu uliitishwa na Baba Mtakatifu Yohane XXIII na kumalizwa na Baba Mtakatifu
Paulo VI. Viongozi 2860 walihudhuria. Lengo kuu la mtaguso huu lilikuwa
kuchunguza na kubainisha wazi nafasi ya Kanisa ulimwenguni, uekumene, upyaisho
wa maisha ya wakfu (kitawa), maisha na utume wa mapadre na nafasi ya walei kama
wadau wa uinjilishaji wa ulimwengu. Yalichunguzwa maboresho ya liturujia.
Mtaguso ulipendekeza Misa iadhimishwe katika lugha mbalimbali badala ya
Kilatini. Mafundisho ya Mtaguso wa Vatikano II yamo katika hati 16: konstitusio
4, dikrii 9 na matamko 3.
Imeandaliwa na Fr. Titus
Amigu
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni