Wakristo wanatakiwa kumuona Yohane mbatizaji kama mfano wa ushuhuda wa unyenyekevu wa Yesu aliyejishusha hadi mauti, ili kuonesha ujio wa Mungu, ni maneno ya Baba Mt. wakati wa Ibada ya Misa katika Kanisa la Mt. Marta akiwahubiri waamini, wakiwemo hata wanandoa waliokuwa wakiadhimisha miaka 50 Sakramenti ya kifungo hicho.
Papa alielezea ya kwamba liturjia ya siku ni kama ya siku zilizopita inayotufanya tutafakari juu ya sura ya Yonane Mbatizaji , katika injili kuwa ni shahidi , na hivyo kwa wito wake ni wa kutoa ushuhuda wa Yesu na taa inayoonesha mwanga , na kutoa ushuhuda wa mwanga. Yeye ni sauti kama ajisevamavyo “mimi ni sauti iliayo nyikani ” Yeye ni sauti lakini anayotoa ushuhuda wa Neno, na kuonesha , Neno la Bwana .Yeye ni sauti tu.Papa aliendelea; Yeye alikuwa ni muhubiri wa toba na akibatiza , lakini alisema wazi ya kwamba “ baada yangu kuna mwingine mwenye nguvu zaidi yangu, na ni mkubwa , ambaye mimi sisitahili kumfunga kamba za viatu na kwahiyo yeye atawabatiza kwa moto na roho Mtakatifu.
Papa aliendelea , mfano wa Yohane ,ni wa muda tu unao onesha kilichokamilika kwa watu na walimu wa sheria walio kuwa wakiuliza kama yeye ni Masiha, lakini aliwajibu ukweli ya kwamba “siyo mimi.”
Aidha papa alisema, ushuhuda wa Yohana uliku wa muda lakini wenye nguvu, wenye mwanga, ambao hakuzimwa na upepo wa majivuno , ni sauti ambayo haikupungukiwa na nguvu au kujidai bali kila siku alikuwa ni kuonesha mlango kwa wengine, aliwafungulia matumaini , huyo ni baba ambaye Yesu katika injili alisema “ mimi ninao ushuhuda mkubwa wa Yohanen wa yule baba”.
Ni Yohane mbatizaji ambaye anafungulia milango ya matumaini, na yeye alisikia sauti ya Baba “ Huyu ndiye mwanangu” .Ni Yohane aliye fungua mlango huo. Papa alisisitiza ya kwamba Yohane ni mkubwa.Ni mnyenyekevu , kwani alichukua njia ambayo hata Yesu alipitia ile ya kujivua mwenyewe, na kuishi hivyo hivyo hata mwisho wa maisha yake ; pale wakati akiwa giza la mahubusu , na baadaye akakatwa kichwa chake , kutokana ahadi za mtoto kucheza ngoma,uliotokana na wivu wa mzinzi na udhaifu wa ulevi.
Papa alitoa mfano ya kuwa ungekuwa unataka kuchora picha hiyo, aliwaambiwa waumini walioudhuria ibada ya misa hiyo ya kwamba; ni hali hiyo tunapaswa kuichora”.
Akiwageukia wote na hasa waliofikisha miaka 50 ya ndoa Papa alisema, ni siku nzuri ya kujiuliza juu ya maisha ya kikristo, je maisha yangu kama mkristo daima yamefungua njia kwa Yesu,je maisha yangu daima yamejazwa na ishala ya kumuonesha Yesu.Na hasa kushukuru zaidi kwa kile alichowatendea , kushukuru na kuanza baada ya miaka 50 ya uzee au ya wa ujana uliozeeka ambao ndiyo divai tamu!
Aliwataka Kufanya hatua mbele ili kuendelea kutoa ushuhuda wa Yesu.Na Yonahe mabatizaji shuhuda mkubwa awasaidie katika njia mpaya wanayoanzaa baada ya kufikia miaka 50 ya ndoa.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican.
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni