0
Solmization ni mfumo au utaalamu au kanuni za kutambua au kutumia silabi ili kutambulisha sauti tofautitofauti katika ngazi (yoyote) step kwa step. Mfumo huu hutumiwa kwenye ngazi za tonic. Asili yake ni huko India to the dif, originated in ancient India.

Mnamo karne ya sita (Mwaka 550-650) Askofu mkuu Isidore, wa Seville alitoa kilio chake kuwa "Kusipokuwa na mfumo wa kukumbuka sauti kwa kuziandika basi nyimbo zitafutika punde." Ndipo mtawa wa kibenediktini Guido akajitosa kwenye kazi ya kuhakikisha tungo / nyimbo takatifu zinawekwa katika mfumo wa kupatikana miaka kwa miaka bila kupoteza uhalisia wake. Guido akiwa mtaalamu wa solmization aliona kuwa nyingi Gregorian chants zilizokuwa maarufu kwa wakati ule zingeweza kufundishika na kueleweka kwa urahisi na waimbaji iwapo wangepewa na kuona tone progression kupanda na kushuka katika ngazi husika ya wimbo, huku mfumo huo ukihusisha sauti (associate it with the sound). Hivyo akatumia au akafikiri kuwa akitumia silabi atapata namna rahisi ya kuimba noti saba za ngazi husika badala ya kutumia majina ya noti (C, D, E, F, G, A, B, C) hapa akatumia silabi do, re, mi, fa, so, la, ti, do kwenye noti za ngazi.
SOL—Fa scale (ngazi ya ki-sol fa) ndiyo jina la mfumo huu.
Haikutokea tu akatumia (akaokoteza) silabi (sauti) hizi, hapana, zilitokana na:-
“Ut Queant Laxis,”
Hymn maarufu ya Middle Ages iliyokuwa ikiimbwa kwenye vespers. Kila mstati uliofuatia katika chant hii ilianza kwa niti moja juu ya noti iliyoitangulia, hivyo Guido alitimia herufi ya kwanza used the first letters of tu kwa kila mstari, na kuwa:-

UT queant laxis,
REsonare fibris,
MI re gestorum,
FA muli tuorum,
SOL ve, nk.

“Ut” baadaye ikaonekana ni ngumu kutamkika hivyo kubadilishwa kuwa “Do.”
Jana, leo na miaka mingi tu huu umekuwa ni mfumo sahihi wa kuimba noti katika sauti.
Thamani ya noti ni twofold
1. Kujua noti yenyewe iwapo ni A ama B ama C ama D na kadhalika. Ila ukiijua kwa jina ni lazima na ukamilishe thamani kwa
2. Kuijua ki-sauti; kwa kuwa noti A itakuwepo kwenye ngazi nyingi, noti B itakuwepo kwenye ngazi nyingi nk.

ASANTE SANA Br. GUIDO. By B. Idama


Chapisha Maoni

 
Top